In Summary

•Mahakama ilidai kuwa haina nguvu ya kuwaeekeza viongozi wakuu wa serikali juu ya mamlaka yao.

Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Image: Facebook//Mike Sonko

Mahakama kuu imekataa ombi la aliyekuwa gavana wa Nairobi, Mike Mbuvi Sonko kutaka kusitisha maandamano ya muungano wa Azimio.

Sonko alikuwa ameomba mahakama kusitisha maandamano ya muungano wa  Azimio kupinga kuongezeka kwa gharama ya maisha na  kushinikiza kufunguliwa kwa sava za IEBC.

Sonko alitaka mahakama iamue kwamba viongozi wa Azimio lazima wafuate masharti ya Sheria ya Utaratibu wa Umma wanapoendesha maandamano hayo. Alisema waandamanaji walikuwa wakiharibu mali, kuharibu biashara na kuvunja amani.

Akidai kuwa baadhi ya waandamanaji walikuwa wamebeba silaha za kuudhi, Bw Sonko, kupitia wakili Harrison Kinyanjui, aliambia mahakama kuwa ombi lake la maagizo ya muda lililenga kulinda haki za wamiliki wa mali na wasioandamana.

Lakini Jaji Hedwig Ong'udi alisema haikuwa kwa mahakama kulazimisha vikosi vya usalama kuhakikisha maandamano ya amani na mkusanyiko kulingana na Sheria ya Utaratibu wa Umma.

“Kifungu cha 6 na 11 cha sheria hiyo kinakataza kumiliki silaha za kivita kwenye mikutano ya hadhara na maandamano. Utekelezaji wa masharti haya yote uko ndani ya hati ya maafisa wa kutekeleza usalama. Ni jukumu la maafisa wasimamizi na wazee wao kuhakikisha kwamba sheria inafuatwa ili kuepuka kukiuka haki za Wakenya,” akasema. 

"Kwa hivyo, haitakuwa sawa kwa mahakama hii kuonekana kuweka kanuni na sera mpya--ambayo haiko ndani ya hati yake. Katika hatua hii, sioni maombi ya maagizo ya kihafidhina kuwa yanafaa. Waache maafisa wanaohusika watekeleze wajibu wao halali. Ombi limekataliwa.”

Alisema Sheria ya Maadili ya Umma pia imeweka kanuni za mikutano ya hadhara na maandamano na mtu yeyote haruhusiwi kushiriki mkutano au maandamano isipokuwa kwa mujibu wa Sheria.

Kuhusiana na kesi ya Bw Sonko dhidi ya tangazo la kiongozi wa Azimio Raila Odinga kuhusu likizo ya umma, mahakama ilishikilia kuwa utaratibu wa kisheria wa kutangaza sikukuu za umma uko tayari.

“Inakuwaje utaratibu huo usipofuatwa? Hiyo ndiyo sababu tunayo  Waziri wa Usalama na masuala ya ndani sna Inspekta Jenerali wa Polisi.  mahakama  hii  haina nguvu ya kuwaelekeza maafisa hawa wawili wakuu wa serikali juu ya mamlaka yao au nani wa kumkamata na nani wasikamatwe. Tuna kanuni inayojulikana kama mgawanyo wa madaraka," mahakama ilisema.

View Comments