In Summary

•Wanasayansi wamepata magonjwa mawili mapya ambayo wanasema hayajawahi kuonekana katika jeni zinazohusiana na kisonono (Gonorea)na klamidia (Chlymadia ).

Image: BBC

Wanasayansi katika Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya (Kemri) wamepata mabadiliko mawili mapya ambayo wanasema hayajawahi kuonekana katika jeni zinazohusiana na kisonono (Gonorea)na klamidia (Chlymadia ).

Miongoni mwa sababu za mabadiliko hayo wamesema ni watu kutotumia kinga wakati wa kujamiana na wengine kuwa na wapenzi wengi.

Ugunduzi huo umewadia huku wachunguzi wakitafuta kuelewa ni kwa nini hospitali mbili katika Kaunti ya Busia, ambayo inapakana na Uganda, zilikuwa na rekodi ya juu ya visa vya magonjwa ya zinaa.

Prof Samson Muuo, msaidizi wa mwanasayansi mkuu wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Mikrobiolojia huko Kemri, alifichua kwamba walishangazwa kupata kwamba wanawake wote 424 wa Kenya walio na umri wa miaka 15 na zaidi ambao chembechembe zao zilifanyiwa sampuli kutoka hospitali hizo mbili walipatikana na ugonjwa wa kisonono na klamidia.

Mwanahabari Anne Ngugi amezungumza na Profesa Samson Muuo na kwanza alimtaka aelezee ugunduzi huo wa magongwa hayo ni hatari kiasi gani  Kenya?

View Comments