In Summary
  • Mwambire alisema iwapo watashuhudia tofauti zozote ndani ya wiki mbili, wataandamana mjini Killifi kutafuta haki.
MCHUNGAJI PAUL MACKENZIE
Image: ALPHONSE NGARI

 MCAs wa Kilifi wametishia kuandamana iwapo mchungaji Paul Mackenzie ataachiliwa kwa dhamana.

Wakiongozwa na Spika wa Kilifi Teddy Mwambire, MCAs walisema ikiwa Mackenzie atapewa dhamana, inapaswa kuwa ya mamilioni au mabilioni.

Mwambire alisema serikali ya kitaifa na seneti inafaa kuangalia kesi ya Mackenzie.

“Mackenzie alifikishwa mahakamani na ukiangalia kesi yake hakimu alikuwa na uamuzi wa kumpa dhamana ya Sh10,000 na wakimtuhumu kwa kesi dhaifu atapewa dhamana ndogo ambayo haitakuwa na msaada. kwetu," alisema.

Mwambire alisema iwapo watashuhudia tofauti zozote ndani ya wiki mbili, wataandamana mjini Killifi kutafuta haki.

"Ikiwa ni lazima kwake kupewa dhamana, anapaswa kupewa kama Sh100 milioni au hata bilioni kwa usalama wake na usalama wa watu wa Kilifi," alisema.

Siku ya Alhamisi, wafuasi 11 wa Mackenzie waliokolewa huku watatu wakiwa katika hali mahututi katika hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi.

Inasemekana kwamba Mackenzie aliwaambia wafuasi wake kwamba kwa kuwa kulikuwa na ukame, wangeharakisha safari yao ya kwenda mbinguni kwa kujiua kwa njaa.

Kasisi huyo na wafuasi wake walifika mbele ya hakimu mkuu wa Malindi Elizabeth Usui lakini hawakushtakiwa huku polisi waliomba muda wa siku 30 kuwashikilia washukiwa ili kukamilisha uchunguzi.

Hakimu alifutilia mbali bondi ya Sh10,000 na kuamuru Mackenzie na wenzake wazuiliwe kwa siku 14 ili kuruhusu polisi kufanya uchunguzi zaidi.

 

 

 

 

 

View Comments