In Summary

• “Watu kama Mackenzie na wengine wote ambao wanafanya vitendo kama vile, hawafai kuwa katika dini yoyote bali ni wageni wa jela tu,” Ruto alisema.

Ruto avunja kimya chake kuhusu pasta Mackenzie.
Image: Facebook

Rais William Ruto kwa mara ya kwanza amevunja kimya kuhusu sakata la mchungaji Paul Mackenzie kuwarubuni waumini wake kujitesa njaa hadi kufa ili ‘kuonana na Mungu’.

Akizungumza mapema Jumatatu asubuhi, rais Ruto alikashfu vitend vya baadhi ya makundi ya kidini ambayo yanajificha ndani ya joho la utakatifu ili kuendeleza visa ambavyo alivitaja kama vya ugaidi.

“Kile ambacho tunaona kule Kilifi ni kitu ambacho hakina tofauti kati ya Mackenzi ambaye anajifanya kuwa mchungaji wakati ukweli yeye ni jambazi sugu. Majambazi hutumia dini kueneza vitendo vyao vya ugaidi na Mackenzie anafanya vile vile,” alisema rais.

Kiongozi wa taifa alidhibitisha kwamba ametoa agizo kwa idara husika kulivalia suala hilo njuga ili kuhakikisha kwamba wote waliohusika wanachukuliwa hatua na kuingia mpaka mizizini mwa jinsi matukio hayo yalivyokuwa yakifanywa.

Rais Ruto alisema kuwa kundi lolote la kidini ambalo litakuwa linatoa mafunzo yanayokwenda kinyume na matakwa ya kikatiba litafungwa mara moja na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Watu kama Mackenzie na wengine wote ambao wanafanya vitendo kama vile, hawafai kuwa katika dini yoyote bali ni wageni wa jela tu,” Ruto alisema.

Sakata la mchungaji Mackenzie limeendelea kuwa gumzo pevu nchini baada ya miili Zaidi ya 40 kufukuliwa na maafisa kutoka idara ya DCI ambao wanaendesha shughuli ya ufukuzi katika shamba la ekari 800 la mchungaji huyo huko Kilifi, Shakahola.

View Comments