In Summary

• Polisi wawasilisha washukiwa 40 wanaodaiwa kuzua vurugu katika mahandamano ya upinzani.

• Polisi walikuwa wamefutilia mbali maandamano ya Azimio kuwa kinyume cha sheria.

Image: TWITTER// DCI

Kufuatia maandamano ya upinzani jamanne tarehe 2, jumla ya watu 40 walikamatwa na polisi kwa madai ya kujihusisha na maandamano ambayo polisi walidai yalikuwa na ghasia.

Wakati wa maandamano hayo, mali yenye thamani ya mamilioni ya fedha iliharibiwa ikiwa ni pamoja na kuchomwa kwa gari la abiria kando ya Barabara ya Ngong na lori lililokuwa likielekea mjini Kampala likiwa na tani 29 za nyaya kwenye barabara ya Southern By-pass.

Washukiwa hao walifikishwa katika mahakama tofauti jijini siku ya Alhamisi na kusomewa mashtaka mbalimbali ikiwemo wizi wa kimabavu, Uharibifu wa mali na miongoni mwa mashtaka mengine.

Miongoni mwa waliokamatwa katika barabara ya Southern By-pass ni Kelvin Kavasika, mshukiwa wa uhalifu  mwenye umri wa miaka 23 na ambaye  alikuwa akisakwa kuhusiana na visa mbalimbali vya ujambazi mjini Naiobi.  

Maafisa wa upelelezi wa DCI pia wamerekodi maelezo kutoka kwa mashahidi mbalimbali na kupata picha za CCTV kuhusiana na baadhi ya matukio ambayo yatawasilishwa mahakamani dhidi ya watuhumiwa.

Polisi katika taarifa kwenye mtandao wa Twitter wamewaonya Wananchi dhidi ya kujihusisha na vitendo vya kihalifu  wakati wa maandamano, waliongeza kuwa atakayekamatwa atachukuliwa hatua za kisheria kibinafsi.

 

 

View Comments