In Summary

• Kindiki pia alisema anahofia kuwa kuna makaburi mengine mengi katika msitu wa Shakahola na hii inawaongoza kuamini kuwa mauaji haya yalikuwa yamepangwa.

• Mshukiwa mkuu wa mauaji hayo, Mchungaji Paul Makenzie Nthenge wa Kanisa la Good News International, anadaiwa kuwaagiza waumini kujinyima chakula ili "kukutana na Yesu."


Waziri Kindiki awasili Malindi kusimamia kurejea kwa shughuli ya ufukkuzi wa maiti Shakahola.

Waziri wa maswala ya usalama Kithure Kindiki amesimamia kurejelewa kwa shughuli ya ufukuzi wa miili ya maiti katika msitu wa Shakahola mapema Jumanne. 

Shughuli hiyo ilikua imesitishwa tarehe 28 mwezi Aprili kwa sababu ya hali mbaya ya anga.

Miili ya watu 112 ilikua tayari imefukuliwa kabla ya kusitishwa kwa muda, ufukuzi huo unarejea baada ya upasuaji wa miili hiyo kukamilika.

Sasa niko hapa kwa sababu ya kusimamia kurejelea kwa ufukuzi wa miili ilivyo amrishwa na koti na ningependa kusema kuwa hadi muda tulipositisha shughuli hii kwa ajili ya hali mbaya ya anga tulikua tumefukua miili 110 kufikia jioni ya siku ile na wengine, pamoja na mmoja aliyefariki akiwa hospitalini na kwa hivyo idadi ya miili iliyofanyiwa upasuaji wa kujua chanzo cha vifo ilikuwa 112”, kindiki alisema.

Kindiki pia alisema anahofia kuwa kuna makaburi mengine mengi katika msitu wa Shakahola na hii inawaongoza kuamini kuwa mauaji haya yalikuwa yamepangwa kwa umakini zaidi.

“Serikali ya Kenya itafanya chochote kitakacho hitajika kufichua matukio ya mauaji katika msitu wa Shakahola.”Kindiki aiongeza.

Mshukiwa mkuu wa mauaji hayo, Mchungaji Paul Makenzie Nthenge wa Kanisa la Good News International, anadaiwa kuwaagiza waumini kujinyima chakula ili 'kukutana na Yesu.'

Alishtakiwa mwezi uliopita baada ya watoto wawili kufa kutokana na njaa wakiwa chini ya uangalizi wa wazazi wao na yuko kizuizini anapongoja kesi yake kuendelea katika mahakama ya Shanzu mjini Mombasa.

View Comments