In Summary
  • Kulingana naye, rais huyo wa zamani alithibitisha kuwa hataachana na siasa na hivyo hafai kufurahia manufaa yanayotokana na kustaafu.
Seneta wa Nandi Samson Cherargei.
Image: STAR

Seneta wa kaunti ya Nandi Samson Cherargei amesema kuwa marupurupu ya Uhuru Kenyatta ya kustaafu yanafaa kukomeshwa mara moja.

Kulingana naye, rais huyo wa zamani alithibitisha kuwa hataachana na siasa na hivyo hafai kufurahia manufaa yanayotokana na kustaafu.

Pia amedai kuwa Uhuru Kenyatta anaweza kuwa anaugua amnesia akisema kuwa alikuwa akitoa vitisho visivyo na nguvu kwa maadui ambao hawapo.

"Nimesikiliza kwa makini hotuba ya Uhuru katika kongamano la kitaifa la Jubilee na nikagundua bado anakataa, anasumbuliwa na amnesia ya kuchagua kutoa vitisho visivyo na nguvu dhidi ya maadui wa kufikirika. Uhuru amethibitisha kuwa hatastaafu kutoka kwa siasa basi Sheria ya Mafao ya Kustaafu ya Rais inapaswa kutekelezwa kwa kuzuilia/ kusitisha marupurupu 100% anayostahiki Rais mstaafu." Samson Cherargei.

Haya yanajiri saa chache baada ya aliyekuwa Mkuu wa Nchi Rais Uhuru Kenyatta kusema kuwa hataachana na siasa.

Uhuru ambaye alikuwa akizungumza wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC) wa Jubilee alisema kwamba hatastaafu kutoka kwa siasa.

“Kuna wakati nilifikiri ningestaafu siasa. Nilidhani wakati ambao ningekuja kwa NDC ungekuwa kukabidhi joho la uongozi." Uhuru Kenyatta alibainisha.

Akizungumza Jumatatu, Uhuru alitilia shaka nia ya Ruto ikiwa anaamini kuwa chama hicho kimekufa.

Mkuu huyo wa zamani wa nchi aliwaambia wajumbe kwamba chama bado kiko imara na kiko hai, hivyo basi maslahi kutoka kwa utawala wa Kenya Kwanza.

Mnasema kwamba chama chetu imekufa, nani ana haja na maiti jamani? Kama imekufa why are you interested? Ukiona wanaitafuta jua haijakufa. We are very much alive na wataiona,"Alisema.

Uhuru alikuwa akijibu majaribio ya chama tawala kutaka viongozi waliochaguliwa wa Jubilee waunge mkono serikali.

Wabunge wanaomuunga mkono Ruto wakiongozwa na mbunge wa EALA Kanini Kega wameunda mrengo wao ndani ya chama na hawamtambui Uhuru kama kiongozi wa chama.

Uhuru wakati wa hotuba yake alitoa wito kwa wale wanaohisi kutoridhika kuwa ndani ya Jubilee kukihama chama hicho na kwenda popote wanapotaka.

Alimkashifu Rais William Ruto kuhusu jaribio la hivi majuzi la 'kuteka nyara' chama cha Jubilee.

Uhuru alisema kuwa hatatikiswa na kutikiswa na vitisho.

"Kuna wale ambao wanadhani kazi yao ni ya vitisho. Lakini sasa wajaribu mwingie , sio mimi,walijaribu kuiba kondoo na kuchoma kichaka wakifikiria tutaogopa lakini waendelee, pia ni haki yao kutoa matusi."

View Comments