In Summary

• Mali ya thamani ya mamilioni ya shilingi iliharibiwa wakati wa moto huo unaosemekana kuanza Jumapili mwendo wa saa nane usiku.

• Ingawa chanzo halisi cha moto huo bado hakijafahamika, wakaazi wanashuku ungeanza kutokana na hitilafu ya umeme.

Moto uliteketeza sehemu ya Soko la Toi huko Kibera mnamo Juni 11, 2023
Image: Twitter

Wafanyibiashara katika soko maarufu la Toi eneo la Kibera Nairobi wanahesabu hasara baada ya moto kuteketeza vibanda katika kisa cha asubuhi.

Mali ya thamani ya mamilioni ya pesa iliharibiwa wakati wa moto huo unaosemekana kuanza Jumapili mwendo wa saa nane asubuhi.

Ingawa chanzo halisi cha moto huo bado hakijafahamika, wakaazi wanashuku kuwa ungeanzia kwa hitilafu ya umeme.

Vyombo vya moto kutoka kwa serikali ya kaunti vilifika eneo la tukio katika juhudi za kujaribu kuzima moto huo ambao ulisababisha mali kuwa majivu.

Hii si mara ya kwanza kwa soko hilo kuteketea kwa moto. Soko hilo limekuwa na tabia ya kuwaka moto mara kwa mara, licha ya serikali kuahidi kukomesha moto huo.

Mnamo Novemba 2021, moto uliteketeza sehemu ya vibanda sokoni, na kuwaacha wafanyabiashara wakihesabu hasara kubwa.

Mnamo 2019, moto  ulizuka sokoni katika muda wa miaka minne baada ya milipuko ya moto ya 2014 ambayo iliharibu mali ya thamani isiyojulikana.

Ukosefu wa barabara za kufikia pia umekuwa na hitilafu kwa mwitikio wa polepole wa huduma za moto.

Mnamo 2018, soko hilo lilikumbwa na visa vitatu vya moto, hali iliyopelekea Rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu kisa hicho na wahalifu wafunguliwe mashtaka.

Mnamo Juni mwaka huo, watu 15 walikufa na takriban 60 kujeruhiwa wakati sehemu ya soko inayohusika na mbao na nguo iliteketezwa.

View Comments