In Summary

• Ruto aliagiza Wizara ya Michezo, Vijana na Sanaa kufanyia mageuzi mfumo wao kuwazawadi wanamichezo bora.

Rais amzawadi Kipyegon shilingi milioni 5 na nyumba ya thani ya shilingi milioni 5
Image: Twitter

Serikali imemtunuku Faith Kipyegon  shilingi Milioni tano pesa taslim na nyumba yenye thamani ya shilingi Milioni 6 kwa kuvunja rekodi mbili za dunia.

Rais alisema kuwa hii itakuwa zawadi kwa rekodi mbili alizovunja katika wa mita 5,000 na mita 1,500.

"Ameshinda na kuvunja rekodi mbili za dunia za mita 1500 huko Florence Italy na ya mita 5000 mjini Paris, Ufaransa. Serikali ya Kenya inakwenda kumzawadia jumla ya Shilingi milioni 5 kwa rekodi moja na tutampa nyumba yenye thamani ya Shilingi milioni 6 kwa rekodi nyingine," Ruto alisema.

Rais aliongeza kuwa itakuwa vivyo hivyo kwa wanariadha wengine watakaovunja rekodi za  dunia watakaofuata baada ya Faith Kipyegon.

"Mkenya yeyote anayeshiriki mashindano ya dunia na kuvunja rekodi, tofauti na siku za nyuma ambapo hakukuwa wanatambuliwa, kwa kila rekodi ya dunia iliyovunjwa serikali ya Kenya inaahidi  kuzawadi shilingi milioni 5," Rais alisema.

Ruto aliagiza Wizara ya Michezo, Vijana na Sanaa kufanyia mageuzi mfumo wao kuwazawadi wanamichezo bora.

"Pia nimeiomba wizara kwamba serikali ya Kenya inafaa kukagua mpango wa zawadi ili tuweze kutambua na kuwatuza ipasavyo wanaume na wanawake wanaofanya vyema katika michezo, sanaa na uchumi wa ubunifu," Ruto alisema.

View Comments