In Summary

• Runinga hii inamilikiwa na Kituo cha kanisa la New Life International linalomikiwa na mchungaji  Ezekiel.

• Kumekuwa na vita mahakamani na Ezekiel akitaka kurejeshwa kwa mawimbi ya runinga ili kumwezesh kupeperusha mahubiri yake.

Mchungaji Ezekiel Odero wakati wa ibada ya Meza ya Bwana Jumamosi.
Image: MAKTABA

Mchungaji Ezekiel Odero amepata ushindi mkubwa baada ya serikali kufungua tena kituo chake cha televisheni kuruhusu wafuasi wake zaidi ya milioni 10 kupata mahubiri yake moja kwa moja.

Televisheni ya World Evangelism ilifungwa mwezi Aprili baada ya serikali kuongeza uchunguzi kuhusu vifo vya Shakahola kutokana na mahubiri ya kidini.

Runinga hii inamilikiwa na Kituo cha kanisa la New Life International linalomikiwa na mchungaji  Ezekiel.

Kumekuwa na vita mahakamani na Ezekiel akitaka kurejeshwa kwa mawimbi ya runinga ili kumwezesha kupeperusha mahubiri yake.

Mhubiri huyo aliambia mahakama kuwa alikuwa akipoteza Shilingi milioni 10  kila wiki kutokana na kufungwa kwa runinga hiyo, jambo ambalo lilimaanisha mamilioni ya waumini wake walishindwa kufuatilia ibada.

Alhamisi, kanisa hilo lilitangaza kufungua tena kituo chake cha televisheni na kumshukuru Mungu kwa hatua hiyo.

"Kwa familia ya Newlife, tunampa Mungu utukufu wote. Sasa tuko hewani katika maruninga ya bila malipo na satelaiti katika nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Kongo na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo," kanisa lilisema.

View Comments