In Summary
  • Alinur ametoa wito kwa Wakenya waweze kumuombea nibu rais Rigathi Gachagua anapoendeleza vita dhidi ya pombe haramu,
ALINUR MOHAMED
Image: KWA HISANI

Waziri Moses Kuria amejipata upande mbaya na Wakenya siku ya Jumatatu hii ni baada ya kushambulia shirika la habari la Nation Media Group.

Mwanasiasa Alinur Mohammed kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter ametoa maoni yake kuhusu ushambulizi dhidi ya Kuria.

Kulingana naye Wakenya wanapaswa kumwombea Moses Kuria kwani huenda amekumbwa na msongo wa mawazo.

Alinur amesema kwamba wanaume wengi wanapitia mambo kwa siri.

"Kila mtu anashughulika kumshambulia Moses Kuria. Lazima kuwe na sababu kwa nini CS wa MITI hajafurahishwa na The Nation Media Group. Hatuwezi kulaumu pombe peke yake. Wanaume hupitia mengi kimyakimya. Labda CS Kuria ana msongo wa mawazo au mambo mengine. matatizo ya kiakili ambayo wanaume wengi wanapigana nayo Kenya.Huenda CS Moses Kuria anapitia changamoto za kifamilia,"Alisema Alinur.

Aidha amesema kwamba atamtafuta waziri huyo ili waweze kuzunguma,pia Alinur ametoa wito kwa Wakenya waweze kumuombea nibu rais Rigathi Gachagua anapoendeleza vita dhidi ya pombe haramu,

"Nitamtafuta na kuzungumza naye ili nijue tatizo lake kuu ni nini.Pia naomba marafiki zetu katika Kenya Kwanza kwa sababu wana maombi sana na wa kiroho, tafadhali tuombee CS wetu Moses Kuria.Labda anapigana vita vya kiroho.Tafadhali muombee DP wetu Rigathi Gachagua anapojaribu kupiga vita ulevi katika nchi yetu.Tuwaombee viongozi wetu kwanza. kuondoa matatizo kutoka kwa maafisa wa serikali kabla ya kufikiria kutoka nje ili kupambana na tatizo ndani ya Wakenya.Nikifaulu kuzungumza na CS Kuria, nitafahamisha ulimwengu.:"

 

 

 

 

 

 

View Comments