In Summary
  • Taarifa fupi iliyoandikwa na mtuhumiwa wa mauaji kwa mtoto wao mkubwa ikiwaelekeza kutumia pesa kwenye simu kumsomesha ndugu yao pia iligundulika.
Crime scene
Image: HISANI

Mwanamume mmoja katika mtaa wa Dandora kaunti ya Nairobi, mbnamo JUmatano alijisalimisha kwa polisi baada ya kumdunga mkewe na kumuua.

Kulingana na ripoti, Tobias Nzola alirejea nyumbani kwake na maafisa wa polisi baada ya kuripoti kwamba alikuwa amemuua mkewe, Agnes Kanini.

Polisi waligundua mwili wa marehemu ukiwa umetapakaa sakafuni, ukiwa na majeraha shingoni na mikononi yaliyoonekana kuchomwa na kitu chenye ncha kali.

Taarifa fupi iliyoandikwa na mtuhumiwa wa mauaji kwa mtoto wao mkubwa ikiwaelekeza kutumia pesa kwenye simu kumsomesha ndugu yao pia iligundulika.

Majirani waliozungumza na waandishi wa habari walisema wanandoa hao walipigana mara kwa mara, hasa baada ya mshukiwa kupoteza kazi mwaka jana.

Wakati huo huo, mwili wa marehemu umehamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City huku uchunguzi ukiendelea.

View Comments