In Summary
  • "Ikiwa nitafanikiwa kufika hapa darasa la saba linapoacha shule basi ninastahili kusherehekewa," Sudi alisema.
Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi
Image: MAKTABA

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi amejibu madai kwamba aliacha shule katika Darasa la Saba.

Alisema hayo siku moja baada ya kikao kirefu cha mahakama ambapo afisa wa uchunguzi alisimulia kuwa alizuru shule zote ambazo Sudi anadaiwa alienda na kubaini kuwa jina lake halikuorodheshwa katika shule zozote isipokuwa shule ya msingi mjini Eldoret.

Afisa huyo, Derrick Kaisha, aliiambia mahakama wakati wa mawasilisho siku ya Jumatano.

Lakini Sudi amesema amefanikiwa kufika mbali baada ya kuacha shule na hivyo basi anapaswa kupongezwa.

"Ikiwa nitafanikiwa kufika hapa darasa la saba linapoacha shule basi ninastahili kusherehekewa," Sudi alisema.

Kaisha alikuwa ameambia mahakama kwamba kutokana na ushahidi uliokusanywa, Sudi hakufanya mtihani wake wa KCSE katika Highway Secondary wala hakusoma KIM ambako alidai kuwa alipata Diploma ya Usimamizi wa Biashara.

Alisema vyeti hivyo vilikuwa na jina lisilo sahihi la shule ya sekondari na namba za fahirisi ni za mtahiniwa mwingine. Pia, saini za cheti cha kumaliza shule zilighushiwa.

"Rekodi pekee tulizopata kuwa mwanafunzi ni katika Shule ya Msingi ya Luok Ngetuny ambapo walimu walithibitisha kwamba alijiandikisha mwaka wa 1995 kwa jina Kipchumba Kipng'etich, lakini alitoka shuleni katika darasa la Saba," Kaisha alisema.

“Hata anwani ya posta aliyoonyesha kwenye cheti cha kuondoka haikuwa ya shule.

"Jina lake halikuwepo popote katika rekodi katika shule na taasisi alizosema alihudhuria," alisema.

Hata hivyo, Sudi amepuuzilia mbali ripoti za vyombo vya habari kwamba aliacha shule.

 

 

 

View Comments