In Summary

• Mbunge huyo alimkosoa DP na kusema matamshi yake hayakufaa na alipaswa kuwaahimiza na kuwamotisha vijana hao.

• Babu owino pia alikosoa serikali kwa kuondoa mpango wa utawala uliopita wa Kazi Mtaani uliokuwa ukiwaajiri vijana.

Mbunge wa Embakasi Mashariki, Paul Ongili almaarufu Babu Owino amemkashifu vikali Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa kuwaambia wahitimu kuwa haitakuwa rahisi kwao kupata ajira..

Akizungumza katika mkutano wa Muungano wa Azimio katika uwanja wa Kamukunji, mbunge huyo alimkosoa na kusema kuwa matamshi hayo ya Naibu Rais hayakufaa na kuwa alipaswa kuwahimiza na kuwamotisha vijana hao.

"Rigathi gachagua aliongea vibaya sana akiwa katika graduation huko JKUAT, alikuwa anasema ati wahitimu hawatapata kazi kwa sababu hakuna kazi, vijana waliwachagua viongozi hawa ili waweze kupata ajira na sasa mnawaambia hakuna kazi.”

Mbunge huyo wa muhula wa pili alibainisha kwamba wazazi walikuwa wakiwekeza pakubwa katika masomo ya watoto wao, kwa hivyo haikuwa sawa kwa Rigathi kuwakufisha moyo wahitimu hao.

"Mtoto ameelimishwa na wazazi wake kutoka slum, amesomeshwa primary, secondary na univeristy bila kufanya uhalifu ama msichana bila kupata mimba na akishamaliza wewe kama DP unaambia huyu mtoto hakuna vile atapata kazi hapa kenya."

Babu owino pia alikosoa serikali kwa kuondoa mpango wa utawala uliopita wa Kazi Mtaani uliokuwa ukiwaajiri vijana kote nchini ili kuweza kusafisha mitaro na barabara katika maeneo wanayoishi na kuweza kupata mapato.

"Youth walikuwa wanafanya kazi mtaani zaidi ya mayouth milioni 5 na vile mliingia statehouse mkatao mpango huo wa kazi mtaani na hio kazi mtaani mlitoa mrudishie ili hawa vijana wapate kazi."

Mnamo siku Ijumaa, Naibu Rais Rigathi Gachagua aliwaeleza bayana wanafunzi wanaotazamia kufuzu kwa nyanja mbalimbali za kazi katika chuo kikuu cha JKUAT, kuwa hataki awadanganye kwamba serikali itawatengenezea nafasi za ajira.

Mimi ni mtu msema ukweli. Sitaki nikae hapa niwadanganye kuwa tuna kazi kwenu. Hizi kazi tutazitengeneza pamoja nanyi. Chuo hiki ni chuo cha sayansi na teknolojia. Wabunge wetu katika bunge la kitaifa kwa usiku mbili walipitisha mswada wa fedha, wenye ushuru wa nyumba. Nyumba 200,000 zinapaniwa kujengwa kila mwaka. Katika nyumba hizo chuo hiki kitatoa wahadisi wa ujenzi, mafundi wa mifereji ya maji, wakaguzi wa ardhi katika ujenzi, na utapata nafasi ya kuishi.

View Comments