In Summary

• Kiswahili ni lugha inayokadiriwa kuzungumzwa na takriban watu  100 milioni kote duniani.

Katika siku hii ya kusherehekea lugha ya kiswahili duniani, tunakumbuka usemi wa kiongozi wa upinzani nchini ya Afrika Kusini Julius Malema akiwahimiza wanaanchi kote Afrika kujifunza lugha ya Kiswahili.

Kiswahili kimeibuka kuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika kutambuliwa na Umoja wa Mataifa na kutengewa siku maalum kuadhimishwa duniani.

Kiswahili ni lugha inayokadiriwa kuzungumzwa na takriban watu  100 milioni kote duniani. 

Baadhi ya mataifa ambayo yanatumia Kiswahili kwa kiwango kikubwa ni Kenya, Tanzania, DRC Congo, Uganda, Msumbiji na Malawi.

 

View Comments