In Summary
  • Kulingana na babake Njenga, Stephen Njoroge, wakati wa usiku wa kisa hicho, maafisa wa polisi waliingia kwa nguvu nyumbani mwendo wa saa 8.00 usiku
Maina Njenga
Image: STAR

Familia ya Maina Njenga inadai kufahamu aliko kiongozi wa zamani wa Mungiki ambaye inasemekana alikamatwa na polisi nyumbani kwake katika Kaunti ya Kajiado Jumatano usiku pamoja na kaka zake wawili na msaidizi wa kibinafsi.

Akihutubia wanahabari nje ya Mahakama ya Milimani mnamo Ijumaa, jamaa ya Njenga alisisitiza kwamba alikamatwa kimakosa huku akiongeza kuwa Serikali inakiuka haki zake za kikatiba kwa kumzuilia kimakosa bila kufichua aliko.

"Hakuna mtu anajua Maina alifanya nini; kwani hii serikali imekuwa aje? Ni nini amefanya adhulumiwe? Tunataka kujua yuko wapi na tunataka haki ya Maina Njenga," Mmoja wa jama za Maina alisema.

"Mtatuambia kwenye yuko. Watu wanaolia hapa ni watoto na bibi wake."

Aliongeza kuwa ilikuwa muhimu kwao kupata ufikiaji wa haraka kwa Njenga kwani afya yake inazidi kuzorota.

"Maina kama ni mgonjwa. Jana tulikuwa tunamtafuta mgonjwa; amekuwa mgonjwa. Hata dawa hiyo hana na hatujui kama anakula."

Kulingana na babake Njenga, Stephen Njoroge, wakati wa usiku wa kisa hicho, maafisa wa polisi waliingia kwa nguvu nyumbani mwendo wa saa 8.00 usiku kabla ya kuwafunga Njenga, kaka zake na msaidizi wake kwenye mojawapo ya magari yao.

“Hii ni kinyume na haki za binadamu. Ni mbaya kwa polisi kuvamia nyumba, kupiga watu bila sababu yoyote,” Njoroge alisema na kuongeza kuwa wafanyakazi wa nyumbani katika nyumba hiyo pia walipigwa na polisi.

Njenga siku za hivi majuzi ameonekana kuwa mkosoaji wa serikali ya Ruto,huku akijiunga na muungano wa Azimion kupinga serikali kuu.

 

 

 

 

View Comments