In Summary

• Uhuru Kenyatta sasa amelazimika kutoa baadhi ya walinzi wake ili kumlinda mamake na aliyekuwa mke wa Rais wa Kwanza,Mama Ngina Kenyatta.

• Jumapili, Rais huyo msattafu alionekana katika uwanja wa Ngong Racecourse akifurahia mashindano ya farasi bila walinzi wowote.

Aliyekuwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Image: screengrab

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta sasa amelazimika kuwatuma baadhi ya walinzi wake kumlinda mamake na ambaye alikuwa mke wa Rais wa Kwanza,Mama Ngina Kenyatta.

Maafisa hao wa polisi waliarifiwa na Uhuru kwenda kuwasaidia walinzi wa kibinafsi waliowekwa katika nyumba ya kibinafsi ya Mama Ngina katika mtaa wa Muthaiga, Nairobi, maafisa wanaofahamu suala hilo walisema.

Haya yanajiri kufuatia uamuzi wa serikali kuwaondoa maafisa wa polisi wa utawala ambao wamekuwa wakilinda nyumba za mke huyo wa rais wa zamani Nairobi na Gatundu.

Uhuru alisema maafisa hao ambao wamekuwa wakimlinda mamake kwa zaidi ya miaka 50 waliondolewa bila maelezo yoyote kwa familia hiyo.

Mama Ngina hakuwepo wakati walinzi hao walipoondolewa mnamo Julai 18.

Hapo ndipo Uhuru aliripotiwa kuwaambia baadhi askari waliokuwa wakilinda kwenda kulinda nyumba ya mamake kufuatia vitisho kwamba wahuni wangevamia.

“Kama watanitaka waje kwa ajili yangu. Niko hapa. Hawapaswi kwenda kwa mama yangu mzee au watoto. Sitatishika. Niko tayari kutetea familia yangu,” alisema.

Jumapili, Rais huyo msattafu alionekana katika uwanja wa Ngong Racecourse akifurahia mashindano ya farasi bila walinzi wowote.

Uhuru alitengamana na wananchi waliokuwa wamehudhuria mashindano hayo kwa uhuru.

View Comments