In Summary
  • Akizungumza na wanachama wa Chama cha Kimataifa cha Wanahabari Afrika Mashariki Jumanne asubuhi, kiongozi huyo wa muungano wa Azimio aliongeza kuwa hazina hiyo itakuwa wazi kwa wengine pia kuchangia .
KINARA WA UPINZANI RAILA ODINGA
Image: TWITTER

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, anasema anapanga kuzindua hazina ya kusaidia "familia zilizopoteza wapendwa wao na wale ambao bado wamelazwa hospitalini wakipokea matibabu" baada ya kujeruhiwa katika maandamano.

Akizungumza na wanachama wa Chama cha Kimataifa cha Wanahabari Afrika Mashariki Jumanne asubuhi, kiongozi huyo wa muungano wa Azimio aliongeza kuwa hazina hiyo itakuwa wazi kwa wengine pia kuchangia .

Maandamano zaidi yalikuwa yamepangwa kufanyika Jumatano kuanzia saa kumi na mbili asubuh hadi saa kumi na mbili jioni lakini, katika taarifa yake kwenye Twitter, Bw Odinga ametaka aina tofauti ya maandamano yafanyike badala yake alisema watafanya mikesha ya kuwakumbuka wahanga wa ukatili wa polisi katika maeneo mbalimbali nchini kote.

"Tunatoa pole zetu kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na ndio sababu tulisitisha maandamano," aliongeza.

Polisi nchini Kenya wamekuwa wakipambana na waandamanaji katika maandamano ya hivi punde ya upinzani kupinga kupanda kwa gharama ya maisha na kupandishwa kwa kodi.

Aidha ilidai kuwa wengi wa waathiriwa walipigwa risasi kwa karibu.

"Wengine wamepigwa risasi mgongoni walipokuwa wakikimbia au wakiwa katika hali ya kujisalimisha. Risasi hizo zimekuwa zikilenga viungo muhimu na sehemu nyeti za waathiriwa kama vile tumbo, mgongo, kifua na kichwa," ilisema.

Kikosi hicho kilisema kuwa waathiriwa hawakuwa na silaha.

Wakati wa mikesha, kuwasha mishumaa na kuweka maua, tunawahimiza Wakenya kufanya maombi na kusoma majina ya waathiriwa wa ukatili wa polisi," ilisema.

Zaidi ya hayo, upinzani uliwataka Wakenya kuomba kwamba Hague inaweza kuingilia kati na kupata haki kwa waathiriwa.

"Tunawaomba Wakenya pia kuomba kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ichukue suala hilo kwa kuzingatia orodha iliyopanuliwa ya wahalifu ambayo tunanuia kuiwasilisha kwa mahakama kwa wakati ufaao," Azimio alisema.

View Comments