In Summary
  • Hali imekuwa ngumu sana huku Wakenya wakisubiri kuona jinsi mzozo kati ya Ruto na Raila utaisha.
RAIS WILLIAM RUTO NA RAIS SAMIA SULUHU
Image: TWITTER

Mvutano wa kisiasa bado uko juu nchini huku madai mapya yakiendelea kutolewa na wanasiasa kutoka kwa mirengo yote.

Mengi yanafanyika na Wakenya wanatazama kwa makini nafasi hii ili kuona njia ya kusonga mbele.

Hali imekuwa ngumu sana huku Wakenya wakisubiri kuona jinsi mzozo kati ya Ruto na Raila utaisha.

Kiongozi wa Azimio Raila siku ya Jumanne alidai kuwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu alikuja Nchini ili kumpatanaisha Rais ruto na Raila ila ruto alimpuuza.

Suluhu alisema kwamba Kenya na Tanzania ni washirika kibiashara.

Akizungumzia walichojadili kwenye mkutano wa leo, Samia Suluhu alisema kuwa;

"Mapema leo katika mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa @WilliamsRuto, pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit), Jijini Dar es Salaam.

Tanzania na Kenya ni washirika kindugu na kibiashara, wakishirikiana mpaka wa urefu wa zaidi ya kilometa 750 wenye umuhimu mkubwa katika ulinzi, usalama na uchumi kwa wananchi wa pande zote mbili."

Huku Ikulu ikijibu madai ya kinara wa Azimio,ilisema kuwa  Ruto hakumualika suluhu.

 

 

 

 

View Comments