logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Waathiriwa wa Shakahola wakulana uroda katika vituo vya uokoaji - DPP

DPP ameelezea hofu kuwa waathiriwa 65 waliookolewa Shakahola wanajihusisha na ngono.

image
na Davis Ojiambo

Habari26 July 2023 - 06:57

Muhtasari


  • • Msaidizi wa mkuugenzi wa mashataka ya umma, alimweleza Hakimu Joe Omide kwamba Serikali inakabiliwa na mzozo mkubwa wa mimba zisizotarajiwa.
  • • Jamii aliiomba mahakama iamuru wahasiriwa hao wahamishwe kutoka vituo vya uokoaji na kupelekwa katika gereza la Shimo La Tewa.

Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma imeelezea hofu kuwa waathiriwa 65 ambao ni mashahidi wakuu katika kesi inayomkabili mhubiri Paul Mackenzie wanajihusisha na ngono katika vituo vya uokoaji.

Msaidizi wa mkuugenzi wa mashataka ya umma, Yamina Jamii, alimweleza Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Shanzu, Joe Omide kwamba Serikali inakabiliwa na changamoto kubwa za mimba zisizotarajiwa na visa vya unyanyasaji wa kijinsia ikiwa waathiriwa wataendelea kuzuiliwa katika kituo cha uokoaji.

"Waathiriwa sasa wamepona kabisa, wana nguvu na wameripotiwa kujamiana. Muda wao mwingi wanautumia kushiriki katika kufanya mapenzi, sambamba na kula na kujumuika kwa uhuru ndani ya vyumba vyao," alisema.

Jamii aliiomba mahakama iamuru wahasiriwa hao wahamishwe kutoka vituo vya uokoaji na kupelekwa katika gereza la Shimo La Tewa ambako watafungwa katika vyumba vya wanaume na wanawake na kusimamiwa kwa urahisi shughuli zao za kila siku.

Mahakama iliambiwa kwamba wawili kati ya walionusurika wana matatizo ya akili, na kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria mara tu familia zao watapatikana.

“Sasa tunaiomba mahakama itowe amri ya kuwapeleka wahasiriwa wote gerezani ili kuepusha mgogoro unaoweza kutokea.

Wahasiriwa hawa waliokolewa kutoka msitu wa Shakahola mwezi Machi mwaka huu baada ya kudaiwa kuingizwa katika dhehebu la mhubiri Mackenzie.

Wakati wakiokolewa, walikuwa wanalazimishwa kufunga ili kuharakisha kifo chao ili waweze kukutana na Yesu.

"Serikali italazimika kushughulikia hata kabla ya kugeuzwa kuwa mashahidi,” alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved