In Summary
  • Watu hao walikuwa wamevamiwa katika nyumba yao na watu wasiojulikana baada ya kufungwa kwa kamba mikononi mwao.
  • Polisi waliotembelea eneo la tukio walisema walimpata Moris Murithi mmoja akiwa amekatwa mkono wa kulia.
Mwanamke mjamzito apatikana amedungwa visu mgongoni
Image: Maktaba//The Star

Polisi wanamsaka mwanamume aliyemkata mkono nduguye katika vita vya kugombania ardhi katika kijiji kimoja kaunti ya Meru.

Kisa hicho kilitokea katika kijiji cha Kaurinene eneo la Antuambui eneo la Igembe na kuhusisha ndugu wawili.

Polisi waliotembelea eneo la tukio walisema walimpata Moris Murithi mmoja akiwa amekatwa mkono wa kulia.

Mshambuliaji wake alikuwa ametoroka eneo hilo. Mwathiriwa alikimbizwa hospitalini na kulazwa akiwa katika hali mbaya.

Pia alikuwa na majeraha makubwa kichwani alipokuwa akipelekwa hospitalini, polisi walisema.

Walioshuhudia walisema wawili hao walipigana kabla ya mshambuliaji kumvamia mwathiriwa katika eneo la kifundo cha mkono na kumkatakata.

Katika eneo hilo hilo, kitongoji cha Kanda, mwanakijiji mmoja aliuawa na shemeji katika vita vya kutaka pesa.

Polisi walisema Josephat Michubu alikatwakatwa na panga kichwani.

Alifariki katika hospitali ya kaunti ndogo ya Nyambene, polisi walisema.

Mwili huo ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri kufanyiwa uchunguzi huku msako wa mshambuliaji ukiendelea. Matukio hayo yalitokea Jumatano jioni.

Polisi wanasema mashambulizi ya aina hiyo ni ya kawaida katika eneo hilo na wanataka wenyeji kutatua mizozo kwa njia ya amani.

Na katika eneo la Jogoo, Kaunti ya Kisii, mwili wa mwanamume ulipatikana kwenye nyumba baada ya kushukiwa kuwa mauaji.

Mwathiriwa wa pili aliokolewa kutoka kwa nyumba hiyo akiwa na majeraha makubwa kichwani na kupelekwa hospitali akiwa amepoteza fahamu.

Watu hao walikuwa wamevamiwa katika nyumba yao na watu wasiojulikana baada ya kufungwa kwa kamba mikononi mwao.

Polisi wanaoshughulikia tukio hilo walisema bado hawajajua sababu za shambulio hilo dhidi ya watu hao wawili.

Polisi wanamsubiri mtu aliyenusurika kupata nafuu na kueleza kilichotokea.

Mwili huo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri kufanyiwa uchunguzi huku msako wa washukiwa ukiendelea.

Matukio kama haya kwa kawaida hufanywa na vikundi vya walinzi vinavyofanya kazi katika eneo hilo kwa ufahamu wa mamlaka, uchunguzi umeonyesha.

 

 

 

 

 

View Comments