In Summary
  • Huku akizungumzia tukio hilo ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alimfumania akiwa anaiwakilisha shule yake 
Seneta wa Nandi, Samson Cherargei
Image: Facebook//Cherargei

Mwanasiasa mashuhuri wa chama cha United Democratic Alliance, Mheshimiwa Cherargei ametaka kukamatwa kwa kocha tapeli ambaye alifichuliwa kwa madai ya kumnajisi msichana ambaye aliahidi kumfundisha.

Katika taarifa ambayo imetolewa na chanzo cha kuaminika, imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alianza kumnajisi mtoto huyo wa darasa la saba.

Huku akizungumzia tukio hilo ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alimfumania akiwa anaiwakilisha shule yake katika mashindano ya mkoa, aliahidi kumsaidia kufika timu ya Taifa kabla ya kuanza kujinufaisha huku akimkumbusha kuwa alimsaidia.

"Alinikuta nikiwa nawakilisha shule yangu na katika harakati hizo, alisema kuwa atanisaidia kufika timu ya Taifa. Alianza kunifaidi baada tu ya kumaliza darasa la 7. Alikuwa akiniambia kuwa yeye ndiye mtu yule yule ambaye atanisaidia na kwa sababu hii aliniuliza kila mara nijisalimishe kwake,"alieleza.

 

Kupitia mitandao yake tofauti ya kijamii alitoa maoni yake kuhusu mada hii, Mwanasiasa  Cherargei ambaye alielezea kusikitishwa kwake na tukio hili amelitaka Jeshi la Polisi nchini kufanya kitu kuhusu hili, kuhakikisha watuhumiwa wanaotumia fursa hiyo kwa wanariadha wa kike wanakamatwa.

"Hiki ni kisa cha kusikitisha cha wanariadha wa kike kunyonywa kingono na kiuchumi na watu wanaojulikana. Natoa wito kwa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai @DCI_Kenya kuangalia kwa haraka suala hili na kuwataka waathirika zaidi kujitokeza ili tusafishe tasnia ya michezo yetu dhidi ya vitendo hivi vya kutisha @moyasa_ke @athletics_kenyaInasikitisha! Hii inasikitisha sana,"Cherargei alitoa wito.

 

 

 

 

View Comments