logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Wanariadha wetu ndio watu pekee wanaopenda Kenya kiukweli,'Donald Kipkorir adai

“Siipendi sana. Lakini yote inahusu kukabiliana, kuamka na kusonga mbele, " alisema.

image

Habari28 August 2023 - 12:02

Muhtasari


  • Kulingana naye serikali inapaswa kulipa Rwanariadha wetu zaidi kwa sababu ndio watu pekee wanaoipenda Kenya kwa dhati.
Mtandao wa kuchumbiana wa Bumble waomba radhi wakili Kipkorir

Wakili Donald Kipkorir amejibu kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter saa chache baada ya Mashindano ya Riadha ya Dunia kukamilika mjini Budapest, Hungary.

Kulingana naye serikali inapaswa kulipa Rwanariadha wetu zaidi kwa sababu ndio watu pekee wanaoipenda Kenya kwa dhati.

"Wanariadha wetu ndio watu pekee wanaoipenda Kenya. Wanafanya mazoezi na kusafiri kwa mbio za riadha kote ulimwenguni kwa gharama zao na kila wakati kuinua bendera yetu". Alisema.

Aliongeza;

"Hao ndio mabalozi wetu wakubwa. Halafu tunawazawadia HSC, Heshima za Kitaifa za chini kabisa wakati wezi wana EBS. Kuna watu walilipwa Mabilioni katika Wizara za Uwekezaji, Mambo ya Nje, Michezo na Utalii kuuza Kenya lakini huwezi kusikia wamefanya nini. .Chapisha Mikataba yao ya Utendaji". wakili Donald Kipkorir aliongeza.

Bingwa wa Dunia katika mbio za mita 1500 na 5000, Faith Kipyegon amefichua kuwa sababu kuu ya mafanikio yake makubwa mwaka huu imekuwa bidii na mazoezi ya kujitolea.

Akizungumza na mwanahabari, mwanariadha huyo wa Kenya mwenye umri wa miaka 29 alifichua kwamba amekuwa akiamka asubuhi sana na kufanya mazoezi kwa bidii huku akijiandaa kwa mbio hizo.

"Nadhani sababu kuu imekuwa mazoezi. Kuamka mapema na kufanya mazoezi, nikilenga msimu bora zaidi,” Faith alisema.

Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za mita 1500 na 5000 alisema kuwa mazoezi ya mbio za masafa marefu imekuwa sehemu ngumu zaidi ya matayarisho yake.

“Siipendi sana. Lakini yote inahusu kukabiliana, kuamka na kusonga mbele, " alisema.

Faith alisema anapenda zaidi mbio za mita 1500 kwani amekuwa akijituma zaidi katika mbio hizo kwa miaka kadhaa.

"Hiyo (mita 1500) ni mtoto wangu kwa sababu nimekuwa nikitazamia rekodi hiyo ya dunia kama miaka mitatu iliyopita na sikufanikiwa. Lakini mwaka huu nimefanikiwa,” alisema.

Wiki iliyopita, Faith Kipyegon alijishindia dhahabu mbili baada ya kuibuka wa kwanza katika mbio za mita 1500 na 5000 katika mashindano ya Dunia yaliyokamilika mjini Budapest, Hungary.

Siku ya Jumamosi, Kipyegon alidhibitisha hadhi yake kama mmoja wa magwiji wa wakati wote kwa kushinda mara mbili katika mji mkuu wa Hungary.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved