logo

NOW ON AIR

Listen in Live

38% ya Wakenya wanaamini kuwa Ruto ametimiza ahadi zake za kampeni-Tifa

Kulingana na Tifa, wahojiwa 1,007 walihojiwa kati ya Septemba 8-10, 2023.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri13 September 2023 - 11:56

Muhtasari


  • Mahojiano hayo yalifanyika kupitia mahojiano ya simu na wahojiwa ambao mawasiliano yao yalikusanywa kupitia ana kwa ana hapo awali.
  • Hata hivyo, ni asilimia 29 tu ya waliohojiwa wanaounga mkono upinzani wanaamini kuwa uimetimiza ahadi yake.

Takriban asilimia 38 ya Wakenya wanaamini kuwa serikali ya Rais William Ruto imetimiza ahadi zake za kampeni.

Katika utafiti wa Tifa, 38% ya Wakenya wanasema wanaamini kuwa serikali ya Ruto imefanya vyema katika kutimiza ahadi zake za kampeni ikilinganishwa na 31% mwezi Juni.

Asilimia 49 ya wanaounga mkono serikali wanaamini kuwa serikali ya Ruto imefanya vyema katika kutimiza ahadi zake za kampeni.

Hata hivyo, ni asilimia 29 tu ya waliohojiwa wanaounga mkono upinzani wanaamini kuwa uimetimiza ahadi yake.

Pia, 32% ya waliohojiwa bila mfungamano wa kisiasa wanaamini Ruto ametimiza ahadi yake.

Kulingana na Tifa, wahojiwa 1,007 walihojiwa kati ya Septemba 8-10, 2023.

Sampuli hiyo ilisambazwa katika kanda 9 zikiwemo Central Rift, Pwani, Mashariki ya Chini, Mt Kenya, Nairobi, Kaskazini, Nyanza, South Rift na Magharibi.

Mahojiano hayo yalifanyika kupitia mahojiano ya simu na wahojiwa ambao mawasiliano yao yalikusanywa kupitia ana kwa ana hapo awali.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved