In Summary

• Taarifa za kifo  cha Aloo ziliripotiwa Ijumaa na inaarifiwa alifariki katika hospitali moja jijini Kisumu akiwa na umri wa miaka 85.

Mamake Chris Musando.
Image: Facebook

Mary Aloo, mamake aliyekuwa mkuu katika kitengo cha ICT kwenye tume ya uchaguzi na mipaka IEBC, Chris Musando amefariki.

Taarifa za kifo  cha Aloo ziliripotiwa Ijumaa na inaarifiwa alifariki katika hospitali moja jijini Kisumu akiwa na umri wa miaka 85.

Kulingana na kijana wake mkubwa Peter Musando, mama yao amekuwa akiugua kwa muda kutokana na shinikizo la juu la damu.

Kwa mujibu wa taarifa, Aloo amekuwa mgonjwa tangu kifo cha ukatili cha mwanawe Chris Musando mwaka 2017 siku chache kuelekea uchaguzi mkuu uliokuwa na ushindani.

Aloo amefariki huku kesi dhidi ya mauaji ya kikatili ya mwanawe ikiwa imejikokota kwa muda mrefu sasa na waliomuuwa wakiwa bado hawajashtakiwa.

Wakati wamaadhimisha miaka 2 baada ya kifo cha Musando, Aloo aliambia Nation kwamba mwanawe alipofariki, alipatwa na mshtuko wa moyo kusababisha tatizo la shinikizo la juu la damu ambalo limekuwa likimsumbua na hakuwa anaweza kutoka kitandani.

“Huwa sitoki kitandani sana, maisha yangu yamebadilika pakubwa, na kuwa mabaya. Kwa kipindi cha miaka miwili sasa, maswali yamejaa kichwani mwangu, ni nani huyu aliyehusika katika kifo cha mwanangu na ni kwa nini?” aliambia Nationa mwaka 2019.

View Comments