In Summary

•Jumamosi jioni, KPLC ilitoa ilani kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa siku ya Jumapili, Novemba 26.

•Katika kaunti ya Kajiado, umeme utatizwa katika sehemu za maeneo ya Ngong, Kibiko na Ngong Kerarapon kati ya saa tatu

Image: MAKTABA

Jumamosi jioni, Kampuni ya Kusambaza Umeme Nchini (KPLC)  ilitoa ilani kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa siku ya Jumapili, Novemba 26.

Katika taarifa yake, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo katika kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Kajiado, Trans Nzoia, Machakos na Uasin Gishu.

Katika kaunti ya Kajiado, umeme utatizwa katika sehemu za maeneo ya Ngong, Kibiko na Ngong Kerarapon kati ya saa tatu. Maeneo hayo yameratibiwa kukosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za barabara ya Kangundo katika kaunti ya Machakos pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Sehemu zitakazoathirika ni pamoja na Kangundo Rd, Joska, Malaa, Koma Hill, Tala, Kangundo, Kikomba, Kyevaluki, Isooni, Kivaani na maeneo ya karibu.

Katika kaunti ya Trans Nzoia, baadhi ya sehemu za maeneo ya Natwana na Makunga zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Maeneo ya Diesel Power na Action katika kaunti ya Uasin Gishu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa nne asubuhi na saa tisa alasiri.

View Comments