logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kindiki avunja kimya kuhusu mauaji ya mwanablogu Sniper

Sniper alitoweka mnamo Desemba 2, kabla ya mwili wake kugunduliwa mnamo Desemba 16.

image
na Radio Jambo

Habari30 December 2023 - 07:01

Muhtasari


  • Katika taarifa yake siku ya Ijumaa, Kindiki alisema wapelelezi wanaochunguza kesi hiyo wanamalizia shughuli ya kuwabaini wote waliohusika katika mauaji yake.

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki sasa anasema kwamba wale wote waliohusika na mauaji ya mwanablogu wa Meru Daniel Muthiani Benard, anayejulikana pia kama Sniper, watafikishwa mahakamani.

Katika taarifa yake siku ya Ijumaa, Kindiki alisema wapelelezi wanaochunguza kesi hiyo wanamalizia shughuli ya kuwabaini wote waliohusika katika mauaji yake.

"Waliohusika na kuandaa, kufadhili na kutekeleza mauaji ya kikatili ya Daniel Muthiani, almaarufu Sniper, wana tarehe na haki.

"Wapelelezi wanahitimisha mchakato wa kuwabaini wahalifu hao, wakiwemo waliomrubuni kijana huyo hadi kumuua na wale waliomtesa, kumuua na kutupa mwili wake kwa nia ya kuficha uhalifu huo mbaya," Kindiki alisema kwenye ukurasa wake rasmi wa X.

Sniper alitoweka mnamo Desemba 2, kabla ya mwili wake kugunduliwa mnamo Desemba 16.

Uchunguzi wa maiti uliofanywa Ijumaa na mwanapatholojia wa serikali Johansen Oduor katika Hifadhi ya Maiti ya Hospitali ya Marimanti Level 4 ulionyesha kuwa Sniper alikufa kwa kunyongwa.

Pia alikuwa amevunjika mbavu na alionyesha majeraha kichwani ambayo yalidokeza kwamba alinyongwa kabla ya kutupwa mtoni.

Baadhi ya Wakenya, wakiwemo maafisa wakuu wa serikali na taasisi wamelaani mauaji ya Sniper na kutaka kukamatwa kwa wale wanaoshukiwa kuhusika na kifo cha Sniper.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved