In Summary

• Raila mnamo Oktoba alitoa dalili wazi zaidi kwamba muungano wa upinzani ungemuunga mkono Musyoka kama kinara wake.

Kalonzo na Odinga.
Image: Facebook

Kwa mara nyingine tena, kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka ameonekana kusisitiza nia yake ya kutomuunga mkono kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, Musyoka alidokeza kwamba hawezi tena kumuunga mkono Odinga kwa uchaguzi wa urais kwa jaribio lake la sita, akisema kwamba safari hii mwenyewe atakuwepo debeni.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 70 alisema kuacha azma yake ya urais tena kwa kumpendelea Raila, kama alivyofanya 2013, 2017, na 2022, itamaanisha kustaafu kutoka kwa siasa kali kwa sababu ya umri wake.

Alijiamini kuwa anaungwa mkono na brigedi ya upinzani, akiwemo Raila, kumng'oa Ruto katika uchaguzi ujao.

Raila mnamo Oktoba alitoa dalili wazi zaidi kwamba muungano wa upinzani ungemuunga mkono Musyoka kama kinara wake.

Hata hivyo, alibatilisha uidhinishaji wake baada ya taarifa yake kuripotiwa kusababisha taharuki kambini. Lakini baadhi ya washirika wa karibu wa Raila wameanza kuungana na Musyoka, na kutoa uthibitisho kwa ripoti kwamba Raila anaweza kuidhinisha ugombea wake.

Pia alitoa wito kwa baadhi ya wanasiasa wa ODM ambao aliwashutumu kwa kumshinikiza Raila kila mara kuwa kwenye kura ili kushinda viti vyao, akisema bado wanaweza kushinda bila waziri mkuu huyo wa zamani kupiga kura.

Musyoka, ambaye alihudumu kama makamu wa rais wa marehemu Mwai Kibaki kati ya 2008 na 2013, alifichua kuwa muungano huo ungeamua mgombeaji wake mapema vya kutosha ili kuepusha mkanganyiko ambao umeharibu michakato kama hiyo hapo awali.

View Comments