In Summary

• Hata hivyo, Ruto alisema kwamba idadi kubwa ya Wakenya haina haja na uhujumu huo kwani wanataka maboresho ya kiuchumi na kimaendeleo.

Rais Ruto
Image: Facebook

Rais William Ruto sasa anadai kwamba mrengo wa upinzani ukiongozwa na Raila Odinga ndio umekuwa katika mstari wa mbele kuhujumu na kulemaza ajenda zake za maendeleo kwa Wakenya katika mwaka wa 2023

Katika ujumbe wake wa Mwaka Mpya kutoka kwa Nakuru State Lodge, mkuu wa nchi alisema kuna kitu kibaya na upinzani wa Kenya.

Rais aliwashutumu kwa kueneza mgawanyiko, migogoro na machafuko nchini, akiongeza kuwa maombi mengi dhidi ya sera zake yanafadhiliwa na watu wenye maslahi binafsi.

"Mtakubaliana na mimi kwamba kuna jambo la kimsingi lisilo sahihi kwa upinzani bila njia mbadala ambayo dhamira yake ni migawanyiko, migogoro na machafuko. Kuna ubaya katika mashauri yanayofadhiliwa na uhujumu kwa lengo la kuchelewesha, kupotosha kuhujumu uwasilishaji wa programu za umma na kuharibu maslahi ya umma,” kiongozi wa nchi alinyoosha kidole cha lawama kwa upinzani.

Hata hivyo, Ruto alisema kwamba idadi kubwa ya Wakenya haina haja na uhujumu huo kwani wanataka maboresho ya kiuchumi na kimaendeleo.

“Mara kwa mara, Wakenya wameonyesha wazi na wazi kujitolea kwao kutafuta fursa za maendeleo kwa kupigia kura sera za kimaendeleo, kama walivyofanya katika uchaguzi uliopita," Ruto alisema.

Mkuu huyo wa nchi aliona kuwa wengi nchini wanazingatia kile ambacho kingechochea nchi kuwa na ukuu.

View Comments