In Summary

• Kati ya watahiniwa hao, 201,133 pekee ndio walipata alama ya C+ kwenda juu, ikimaanisha kwamba watajiunga na vyuo vikuu baadae mwaka huu.

Waziri Machogu atoa matokeo ya KCSE 2023.
Image: X

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu mapema asubuhi ya Jumatatu 8, alitangaza rasmi matokeo ya mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne.

Machogu ambaye alitangaza matokeo hayo kutoka shule ya upili ya wasichana Moi mjini Eldoret alisema watahiniwa 889, 453 waliketi mitihani hiyo.

Kati ya watahiniwa hao, 201,133 pekee ndio walipata alama ya C+ kwenda juu, ikimaanisha kwamba watajiunga na vyuo vikuu baadae mwaka huu.

Hii ni sawa na asilimia 22.27 ya watahiniwa wote ambao walifanya mitihani hiyo ya KCSE, ikiwa ni asilimia ya juu Zaidi kulinganishwa na mwaka 2022 ambapo 19.67% sawa na wanafunzi 173,345.

“Idadi ya watahiniwa waliopata sifa ya chini zaidi ya kuingia chuo kikuu (Daraja C+ na zaidi) ilikuwa 201,133 (22.27%) katika Mtihani wa KCSE wa mwaka wa 2023 ikilinganishwa na 173,345 (19.62%) mwaka wa 2022. Hii ni kutokana na maombi ya mfumo mpya wa kuweka alama,” alisema Machogu.

Kulikuwa na watahiniwa 1,216 (0.14%) waliopata jumla ya daraja A katika Mtihani wa KCSE wa mwaka wa 2023 ikilinganishwa na watahiniwa 1,146 (0.13%) mwaka wa 2022.

Idadi ya watahiniwa wenye umri wa miaka 16 na chini iliongezeka kutoka 12,710 (1.438%) mwaka wa 2022 hadi 16,040 (1.776%) mwaka wa 2023. Asilimia kubwa zaidi ya watahiniwa waliosajiliwa kwa Mtihani wa KCSE wa 2023 walikuwa ndani ya umri ufaao wa kati ya Miaka 17 hadi 19.

View Comments