KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Februari 1.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Kajiado, Uasin Gishu, Busia na Meru.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu ya eneo la Nairobi West na sehemu ya barabara ya Lang'ata zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za eneo la Rongai katika kaunti ya Kajiado pia zitakuwa bila stima kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Uasin Gishu, sehemu za maeneo ya Cheplaskei, Outspan, Kabiyet, Ndalat, Kaiboi na Mlango zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu na saa kumi alasiri.
Sehemu ya kaunti ya Busia katika maeneo ya Amase na Among'ura itakosa umeme kati ya saa tatu na saa kumi na moja jioni.
Wakati huohuo, sehemu za maeneo ya mji wa Meru, Thimangiri na Giaki zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.