In Summary

• Kiongozi wa taifa alisema kwamba sehemu nyingi zinazokumbwa na changamoto za kiusalama nchini kama Baringo, West Pokot za zingine ni kutokana na uhaba wa injili ya kuwakomboa majangili wanaoiba mifugo na kuua wananchi.

RUTO
Image: FACEBOOK

Rais William Ruto ametoa wito kwa kanisa kutoa msaada wao katika kuhakikisha changamoto za kiusalama katika maeneo mbalimbali nchini zinatokomezwa.

Akizungumza katka hafla ya kanisa la PCEA jijini Nairobi, aliomba kanisa hilo kutuma wamishenari wengi katika maeneo mbalimbali nchini Kenya ambayo yako katika hatari za kiusalama kama vile sehemu za Pokot Magharibi, Baringo, Kerio Valley ambako wezi wa mifugo wamekuwa wakiwahangaisha wananchi kila uchao.

Kiongozi wa taifa alisema kwamba sehemu nyingi zinazokumbwa na changamoto za kiusalama nchini kama Baringo, West Pokot za zingine ni kutokana na uhaba wa injili ya kuwakomboa majangili wanaoiba mifugo na kuua wananchi.

“Bado tunahitaji pesa ya kueneza neno. Kuna watu hawajafikiwa na neno la Mungu. Hata yale matatizo ya wezi wa mifugo tuko nayo kule West Pokot na sehemu zingine, tatizo kubwa ni vita vya kiroho,” Ruto alisema.

“Tunataka PCEA kutuma wamishenari Zaidi katika sehemu za ndani kabisa za Kenya, kwa sababu matatizo katika sehemu hizo kati yake ni matatizo ya vita vya kiroho na tunahitaji jeshi la kiroho kupambana nayo. Tunaweza kufanya kile ambacho tunaweza sisi kama serikali, lakini vita ya kiroho inataka jeshi la kiroho kupambana,” alimaliza.

Kauli hii inakuja siku chache baada ya kutoa tamko kali kwa magenge ya wizi wa mifugo kaunti ya West Pokot alipozindua kiwanda cha Cemtech Clinker cha kutengeneza saruji cha mjasiriamali bilionea, Narendra Raval.

 

View Comments