In Summary

• Natembeya alisema kwamba KDF wanafaa kupelekwa katika eneo hilo na kupewa kipindi cha miezi 3 tu, na suala la utovu wa usalama litakuwa limetokomezwa kikamilifu.

gavana george natembeya
Image: hisani

Gavana wa Trans Nzoia ambaye pia aliwahi kuwa kamishna wa eneo pana la Bonde la Ufa, George Natembeya ameshauri njia ya kumaliza ujahili na utovu wa usalama katika eneo la kaskazini mwa Bonde la Ufa ni kutuma vikosi vya jeshi la KDF.

Natembeya alitoa ushauri huu kupitia kipindi cha News Court kwenye runinga ya NTV ambapo walikuwa wanajadili suala la utovu wa usalama katika kaunti za North Rift.

Natembeya ambaye alihukumu kama RC wa Bonde la Ufa kwa takribani miaka 2 na nusu kabla ya kujiuzulu na kujitika katika siasa alisema kwamba kama kweli rais Ruto ana azma ya kumaliza ujahili kaitka eneo hilo, dawa pekee ni kupeleka vikosi vya KDF.

Natembeya alisema kwamba KDF wanafaa kupelekwa katika eneo hilo na kupewa kipindi cha miezi 3 tu, na suala la utovu wa usalama litakuwa limetokomezwa kikamilifu.

“Ambacho serikali inastahili kufanya ni kwenda bungeni na kupata kibali kinachohitajika kutoka kwa bunge la kitaifa, cha kupelekwa kwa jeshi katika North Rift, acha jeshi lichukue usukani wa oparesheni hiyo kikamilifu, maafisa mengine wa polisi wakiwa wamevalia raia watakuwa wanatoa msaada kwa jeshi, kama kuwaondoa watu waliojeruhiwa, kuwaahimisha raia kutoka sehemu za kushambuliwa na KDF,” Natembeya alieleza.

“Patia jeshi miezi 3, kikamilifu wakiwa na kila kitu, na usalama utapatikana,” aliongeza.

Natembeya kabla ya kujitosa kwenye siasa na kushinda kiti cha ugavana Trans Nzoia, alikuwa amehudumu kwenye umma kwa kipindi cha miaka 26.

View Comments