In Summary

•Wakenya kuwasilisha maoni yao kuhusu muswada wa sheria  ya fedha kupitia barua pepe

•Siku ya mwisho kuwasilisha ni Mei 28,2024 saa kumi na moja jioni.

Bunge la Kenya
Image: Twitter @NAssembly Kenya

Kamati ya Idara ya Fedha na mipango ya kitaifa imetoa wito kwa raia wa Kenya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kutunga sheria kwa kuwasilisha maoni yao kuhusu mswada mpya wa Fedha wa 2024.Wakenya wanaweza wasilisha maoni yao kwa kuandaa risala,ambayo inaweza wasilishwa kimwili au kutumwa kupitia barua pepe.

Hii itahakikisha kwamba mchakato wa kutunga sheria unakuwa wa uwazi na unazingatia michango ya wadau wote.

'Kwa kuzingatia ibara ya 118[1] [b] ya katiba na kanuni ya kudumu ya 127[3], katibu wa bunge anakaribisha umma na wadau kuwasilisha risala za miswada kwa kamati ya idara ya fedha na mipango ya kitaifa...' taarifa hiyo ya bunge ilisema.

Mswada huo unapendekeza marekebisho katika vipengele kadhaa muhimu vya sheria,ikiwa ni pamoja na sheria ya ushuru wa mapato,sheria ya kodi ya ongezeko la thamani,na sheria ya ushuru wa bidhaa amabayo itaathiri ustawi wa kiuchumi na kifedha wa wakenya wote.

Mswada huo pia utaathiri sheria kama vile sheria ya makazi ya nafuu,sheria ya mafunzo ya viwandani, na sheria ya kulinda data ,ikionyesha athari za maisha na biashara ya wakenya hivo kila mkenya anashauriwa kutoa maoni yake.

View Comments