In Summary

•Idadi kubwa ya wanafunzi wakimbilia kozi za diploma

•Kozi za matibabu kwa shahada ya chini zapokea wanafunzi wengi.

Lango la Chuo Kikuu cha Kenyatta
Image: MAKTABA

Kuna ongezeko la idadi ya wanafunzi waliofuzu kujiunga na vyuo vikuu kususia nafasi zao na badala yake kujiunga vyuo vya kadri kusomea diploma. 

Kulingana na ripoti iliyotolewa na  mamlaka ya kuwachagua wanafunzi kujiunga na vyuo nchini KUCCPS Jumla ya wanafunzi 47,872 hawakutuma maombi kujiunga na vyuo vikuu na badala yake wakachagua kujiunga vyuo vya diploma.

Vyuo vikuu vina uwezo wa jumla wa 278,006 kwa programu za digrii ila ni wanafunzi 153,274 pekee waliowekwa kati ya 201,146 waliohitimu kuandikishwa.[asilimia 55] Ushindani wa kozi katika vyuo vya mafunzo vya matibabu 'KMTC' pia umeongezeka baada ya watahiniwa 56,516 kutuma maombi ya kuandikishwa katika kozi hizo za matibabu.

Zaidi ya hayo wanafunzi 199,980 wamepangiwa kozi za stashahada,huku waliopata alama za wastani za D+ na D - na E takriban 213,932wakisomea kozi za ufundi.

Jumla ya matokeo ya watahiniwa 899,232 yaliwasilishwa kwenye huduma ya kupanga wanafunzi katika vyuo vikuu ili kupangwa.

Ni kwa nini wanafunzi wengi wanalenga kozi za diploma hata baada ya kufuzu vizuri ikilinganishwa na zile za shahada?

View Comments