In Summary

•Cleophas Malala ameunga mkono ajenda ya Tawe Movement inayoongozwa na Gavana George Natembeya wa Trans Nzoia.

•Natembeya aliwashutumu Mudavadi na Wetang'ula kwa kukosa kuleta maendeleo ya Magharibi licha ya kuwa serikalini kwa miongo kadhaa.

Katibu mkuu wa UDA Cleophas Malala
Image: Facebook

Katibu Mkuu wa Chama cha United Democratic Alliance (UDA) Cleophas Malala ameunga mkono vuguvugu la Tawe la gavana wa Trans Nzoia George Natembeya.

Akizungumza katika kaunti ya Vihiga, Malala alisema anaunga mkono kikamilifu ajenda inayoongozwa na Natembeya, inayotaka katibu mkuu wa baraza la mawaziri Musalia Mudavadi na spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang'ula kustaafu kutoka kwa siasa.

Malala alimtaka Natembeya kuwaongeza aliyekuwa gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya na aliyekuwa waziri wa ulinzi Eugene Wamalwa kwenye ajenda za vuguvugu hilo.

"Naunga mkono kikamilifu ajenda yako huko Trans Nzoia; nimeona ukiwasukuma Wetang'ula na Mudavadi waende nyumbani. Hata hivyo, orodha haijajaa; hata Oparanya na Eugene wanafaa kwenda nyumbani kupumzika," Malala alisema.

Aidha Malala pia alikashifu mpango wa Oparanya kuwania useneta wa Kakamega 2027. Malala alisema ni wakati wake wa kupumzika kutoka kwa siasa, kwani amekuwa mamlakani tangu enzi za Ford Asili.

Baadhi ya wanasisa kama  vile mbunge wa UDA Gathoni Wamuchomba pia  wameunga mkono ajenda ya Gavana Natembeya. 

View Comments