In Summary

•HELB imefungua rasmi tovuti yake ya maombi ya  fedha 2024-2025 kwa wanafunzi ambao wanajiunga na vyuo vikuu na vile vya kiufundi kwa mara ya kwanza.

•Wanafunzi wanaweza tembelea tovuti https://www.hef.co.ke/

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HELB) imetangaza rasmi kufungua tovuti yake ya maombi ya mikopo mwaka 2024-2025.

Tovuti hio imefunguliwa kwa mara ya kwanza kwa wanafunzi wanaowania masomo ya shahada ya kwanza pamoja na wale wa  mafunzo ya ufundi (TVET).

Mpango huu unalenga kutoa usaidizi wa kifedha kwa wanafunzi wapya ambao watajiunga katika vyuo vikuu na taasisi za TVET chini ya wizara ya elimu kwa kuzingatia mtindo mpya wa ufadhili. [HEF]

Wanafunzi wanatakiwa kuwa na barua pepe halali, nambari ya simu, nambari za 'index' za KCPE na KCSE, na picha ya ukubwa wa pasipoti, miongoni mwa mambo mengine.

HELB ilitangaza kuwa wanafunzi wanaostahiki wanaweza kutuma maombi ya ufadhili wa masomo na mikopo kupitia tovuti rasmi ya HELB, kwa https://www.hef.co.ke/ baada ya kuhamishwa kutoka kwa helb.

Chini ya mpango huo mpya, HELB inalenga wanafunzi wa mara ya kwanza waliodahiliwa katika vyuo vikuu na vile vya kiufundi  katika taasisi zinazotambuliwa na wizara ya elimu.

View Comments