In Summary

•Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Makueni, Uasin Gishu, Migori na Nyeri.

Kenya Power
Image: HISANI

Kampuni ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya ijumaa, Juni 21

Katika taarifa ya Alhamisi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Makueni, Uasin Gishu, Migori na Nyeri.

Katika kaunti ya Makueni, eneo la Mombasa road litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Osori na Sori katika kaunti ya Migori yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Uasin Gishu, baadhi ya sehemu za maeneo ya Kapseret na Lemook zitakosa umeme kati ya saa tatu na nusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Nyeri, baadhi ya sehemu za maeneo ya  Mbiriri na Karundas zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

View Comments