In Summary

•Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Rongo alithibitisha kisa hicho huku akiomba usaidizi katika shughuli ya uokoaji.

•Wengine wanne wanapokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Rongo.

crime scene

Watu wawili wamethibitishwa kufariki baada ya ukuta wa mgodi wa dhahabu wa mita 750 kuporomoka huko Kanga, Kaunti ndogo ya Rongo, Migori.

Wachimba migodi 18 walikuwa kazini kwenye mgodi wa dhahabu wa Choppa wakati kuta zilipoporomoka. Zaidi ya watu 10 bado wamekwama katika mgodi huo huku juhudi za kuwaokoa zikiendelea.

Wengine wanne wanapokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Rongo.

Kulingana na naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Rongo George Otenga, watu 18 walikuwa kwenye mgodi huo kabla ya kuporomoka.

Naibu kamishna wa kaunti vile vile alisema kuwa serikali ya kaunti ya Migori imekusanya wafanyikazi na rasilimali kusaidia kuwaokoa wale ambao bado wamekwama ndani ya mgodi huo.

Serikali ya kaunti inasalia na matumaini kuwa itafanikiwa kuwafikia watu walionaswa hivi karibuni.

Tutakuletea taarifa zaidi.

View Comments