logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Viongozi walioandamana na Ruto kanisani Bomet wanyimwa nafasi ya kuongea

“Viongozi wetu mliopo leo naomba msimame popote mlipo...tunashukuru mmekuja,” alisema.

image
na Davis Ojiambo

Habari21 July 2024 - 14:30

Muhtasari


  • • Waziri mteule wa Barabara Davis Chirchir mteule aliyeunga mkono kikamilifu ujenzi wa kanisa hilo pia alikuwepo.
  • • Askofu Robert Langat ambaye aliongoza ibada hiyo alitambua tu uwepo wao na akamwalika Ruto kuzungumza.
RUTO

Katika hali nyingine inayoendelea hivi majuzi na viongozi wa kanisa, wanasiasa walioandamana na Rais William Ruto wakati wa ibada ya kanisa huko Bomet leo walinyimwa fursa ya kuzungumza.

Ruto alikuwa Sotik kwa ufunguzi rasmi na kuwekwa wakfu kwa kanisa jipya la Chebango AGC.

Gavana Hillary Barchok ambaye alikuwa mwenyeji wa rais pia alinyimwa nafasi ya kuzungumza.

Miongoni mwa viongozi waliochaguliwa waliohudhuria ni Seneta Hillary Sigei, Mbunge wa Dagoreti kusini John Kiarie, Mwangi Kiunjuri (Laikipia Mashariki), Francis Sigei (Sotik), Brighton Yegon (Sotik) na kamishna wa JSC Isaac Rutto.

Waziri mteule wa Barabara Davis Chirchir mteule aliyeunga mkono kikamilifu ujenzi wa kanisa hilo pia alikuwepo.

Askofu Robert Langat ambaye aliongoza ibada hiyo alitambua tu uwepo wao na akamwalika Ruto kuzungumza.

“Viongozi wetu mliopo leo naomba msimame popote mlipo...tunashukuru mmekuja,” alisema.

“Tunawapenda sana waheshimiwa wetu, mungu awabariki,” alisema.

Akiongea, Ruto alisema wamekubali kuheshimu kanisa kama mahali patakatifu pa ibada.

"Kanisa ni mahali patakatifu tutaheshimu na maneno yale mengine ya kisiasa tutafanya ndiyo tuweke heshima kwa kanisa vile inavyofaa," alisema.

Hii inatafsiriwa kuwa, "kanisa ni mahali patakatifu na tutalipa heshima inayostahili, tutapeleka siasa zetu nje ya kanisa kwa heshima hiyo."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved