In Summary

•Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanywa kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Bomet, Trans Nzoia, Kisii,Nyamira, na Nyeri.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Julai 22. 

Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanywa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Bomet, Trans Nzoia, Kisii,Nyamira, na Nyeri.

Katika kaunti ya Bomet, sehemu kadhaa za maeneo ya Kiromwok na Kitoben yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kaplamai na Nyakinywa katika kaunti ya Trans Nzoia yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kisii, sehemu za eneo la Mogumo zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu za mji wa Nyamira na Kebirigo katika kaunti ya Nyamira zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhina saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Chorongi na Skuta katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

View Comments