In Summary

•Njeri Mwangi ameomba msamaha kwa kutopatikana kwenye simu wakati watu walipokuwa wakiwatafuta ili kuwajulia hali.

•Siku chache zilizopita, mwanaharakati huyo alifunga akaunti zake zote za mitandao ya kijamii ambayo ina wafuasi wengi sana.

Bonface Mwangi na Mkewe Njeri
Image: Boniface Mwqangi (Facebook)

Bi Njeri Mwangi, mke wa mwanaharakati maarufu nchini Kenya Boniface Mwangi hatimaye ametoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kufuatia wasiwasi uliojitokeza kuhusu hali ya mumewe.

Katika chapisho la Jumatatu asubuhi, mama huyo wa watoto watatu aliomba msamaha kwa kutopatikana kwenye simu wakati watu walipokuwa wakiwatafuta ili kuwajulia hali.

Pia alitoa shukrani zake kwa upendo na sapoti nyingi ambazo familia yake imepokea katika siku chache zilizopita za kutisha.

“POL🙏🏾 Marafiki na wandugu, samahani kwa simu zisizopokelewa na meseji ambazo hazikujibiwa. Tafadhali mnisamehe na mnivumilie. Tunahisi upendo na sapoti yenu safi inayomiminika. Tunashukuru yote  Asante,” Njeri aliandika kwenye mtandao wa Twitter.

Image: TWITTER// NJERI KAN

Haya yanajiri wakati Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameendelea kuibua wasiwasi wao kuhusu hali ya mwanaharakati Boniface Mwangi.

Siku chache zilizopita, mwanaharakati huyo alifunga akaunti zake zote za mitandao ya kijamii ambayo ina wafuasi wengi sana. Hii ilikuja muda mfupi baada ya kuchapisha ujumbe wa kutia wasiwasi kuhusu kitendo cha kujitoa uhai.

"Hakuna kitu cha ubinafsi kuhusu kujitoa uhai. Mtu anafikia hatua maishani, na anaamua hii ni kwao. Wako tayari kwa ulimwengu ujao. Maumivu, shida, na matarajio ya wengine katika ulimwengu huu ni mengi sana. Wanatoka jukwaani. Sherehekea maisha yao. Mwisho wa hadithi,” Boni aliandika kwenye Facebook wiki jana kabla ya kutoweka mtandaoni.

Aliambatanisha posti yake na picha yake.

Hatua hiyo ilizua mazungumzo makubwa mtandaoni huku wengi wakieleza wasiwasi wao kuhusu hali yake.

 Mwanaharakati mwenzake Hanifa Farsafi baadaye alithibitisha kuwa amemwona, na alikuwa sawa.

View Comments