Katibu Mkuu wa Masuala ya Kigeni, Korir Sing’oei, sasa anataka Serikali kudhibiti kwa uthabiti mikutano na maandamano nchini Kenya akitaja changamoto za kiuchumi zilizosababishwa na shughuli hizi.
Katika taarifa kwenye akaunti yake ya X, PS huyo alibainisha kuwa maandamano, mara nyingi yanayojumuisha kaumu kubwa ya watu, yameathiri uchumi hasa katika sekta binafsi.
“Sehemu ya sababu ya kudhibiti na kushughulikia maandamano yenye ghasia na machafuko ni kwamba waandamanaji hawatambui gharama za vitendo vyao,” alisema.
“Gharama hii inahamishiwa na kubebeshwa mtu mwingine - sekta binafsi. Kama uchafuzi wa mazingira, maandamano yenye ghasia yanapaswa kudhibitiwa kabla hayajasababisha gharama za umma zisizoweza kurekebishwa.”
Matamshi yake yanakuja siku moja tu kabla ya vijana wa Kenya kupanga kupiga hatua mitaani kwa lengo la kusukuma mageuzi na mapinduzi nchini Kenya.
Maandamano hayo yanakadiriwa kuzuka na makovu yake yanazidi kushuhudiwa na kuhisiwa kila kunapokucha.
Mpaka sasa, takriban zaidi ya wakenya hamsini hasa wengineo vijana na watoto wachanga wameripotiwa kufariki huku wengine wakitekwa nyara.