logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tazama kaunti 7 zitakazoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Alhamisi

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Kiambu, Nakuru, Kisumu, Nyeri, Embu, Meru na Kwale.

image
na Samuel Maina

Habari08 August 2024 - 04:24

Muhtasari


  • •Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Kiambu, Nakuru, Kisumu, Nyeri, Embu, Meru na Kwale.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Agosti 8. 

Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Kiambu, Nakuru, Kisumu, Nyeri, Embu, Meru na Kwale.

Katika kaunti ya Kiambu, maeneo ya Wangige na Mwimuto yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Chuo Kikuu cha Egerton katika kaunti ya Nakuru litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maenelo ya mji wa Kibos na Kirdi katika kaunti ya Kisumu yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Katika kaunti ya Nyeri, maeneo ya Ihithe, Hubuini, na Kina yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Mugoya na Njakairi katika kaunti ya Embu yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.

Sehemu za mji wa Meru na Thimangiri zitakosa katika kaunti ya Meru zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za mji wa Kwale na Kinango katika kauntiya Kwale pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved