logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo ambayo yatakosa umeme leo, Jumatatu

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Homa Bay, Nyeri, Murang'a, Kiambu.

image
na Samuel Maina

Habari12 August 2024 - 04:49

Muhtasari


  • •KPLC imesema baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Homa Bay, Nyeri, Murang'a, Kiambu.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Julai 29. 

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Homa Bay, Nyeri, Murang'a, Kiambu.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Kilimani, Argwings Kodhek na barabara ya Ngong zitakiosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Ogandi Girls, Ndiru, na Arujo katika kaunti ya Homa Bay yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Miagayuini, Ngooru, Zaina, Jua Kali na Ihwagi katika kaunti ya Nyeri yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Murang'a, sehemu za maeneo ya Maragua, Ichagaki, Nginda, na Gachocho zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Kariminu Dam, Naivasha Road, na Ituramiro Rd katika kaunti ya Kiambu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved