logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tazama kaunti 7 zitakazoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Jumanne

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Mombasa, Kajiado, Kisumu, Nyeri,Homa Bay na Bungoma.

image
na Samuel Maina

Habari13 August 2024 - 04:20

Muhtasari


  • •KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Mombasa, Kajiado, Kisumu, Nyeri,Homa Bay na Bungoma.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Agosti 13. 

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Mombasa, Kajiado, Kisumu, Nyeri,Homa Bay na Bungoma.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Kibiku Feeder, Ruai Sewage, Joska Feeder, Utawala, Njiru, Vicken Feeder, North Impact, KCC Village, Bomas of Kenya na Galleria zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Kitengela na Isinya katika kaunti ya Kajiado zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Sondu, Nyabondo, na Sigoti katika kaunti ya Kisumu yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Maeneo ya Khachonge, Bwake, na Luuya Girls katika kaunti ya Bungoma yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Katika kaunti ya Nyeri, maeneo ya Amboni Dairy, Laini Saba, PCEA Amboni, Wendiga, na Kiguru yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Ogandi Girls, Ndiru, na Arujo katika kaunti ya Homa Bay yataathirika kati ya saa tatu na saa kumi alasiri.

Eneo la Mshomoroni katika kaunti ya Mombasa pia litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved