KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Agosti 14.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kakamega, Nyeri, Homa Bay, Bungoma, Murang'a, na Isiolo.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mitaa ya Karen na Ngong Rd zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Ekonjero na Hospitali ya Muhila katika kaunti ya Kakamega yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Bokoli, Matisi, na Bukembe katika kaunti ya Bungoma yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa nane alasiri.
Maeneo ya Wangapala, Asumbi, Mfangano Island, na Rangwe katika kaunti ya Homa Bay yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Soko za Gikumbo na Gaikuyu katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa nane asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Murang'a, maeneo ya Kabati, AAA Growers na Pro Gas yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Maili Saba, Maili Tatu, Archers Post, Sarova na Wamba katika kaunti ya Isiolo pia yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.