Sehemu ya wabunge wameapa kujiunga na maandamano ya Gen Z ambayo yanatarajiwa kurejelewa kuanzia Jumanne wiki ijayo.
Wanasiasa hao vijana ambao wengi wao ni kutoka mrengo wa upinzani wanadai kwamba rais William Ruto angali bado hajatekeleza mageuzi na mabadiliko ambayo yamekuwa yakishinikizwa na vijana wa Gen Z tangu maandamnao hayo yalipolipuka mwezi Juni mwaka huu.
Wakiongozwa na mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na mwenzake wa Githunguri Gathoni Wamuchomba, wabunge hao walisema kwamba Ruto hajaonyesha nia ya kutatua masuala ibuka kama ukosefu wa kazi, gharama ya juu ya maisha.
“Tungependwa kukuambia rais Ruto usiwajaribu watu wa Kenya kupita kiasi, wamekupa nafasi ya kupitia upya vipaumbele vyako na kuipata njia sahihi. Wameshangazwa kwamba bado hujarekebisha kitu chochote,” Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino alisema.
“Acha tuhakikishe tunasukuma haya mapambano zaidi kwa sababu hakuan suluhu limepatikana mpaka sasa,” aliongeza mwenzake wa Starehe, Amos Mwago.
Aidha, Catherine Omanyo, mwakilishi wa kike kaunti ya Busia alimsuta Ruto kwa mwenendo wa kuzindua miradi mingi isiyokamilika na miraid mingine ambayo ilizinduliwa hapo awali
“Mnaeza ona pahali ambapo roho yake ipo, kuonesha PR nyingi na miradi midogo midogo ndio anazindua lakini kitu ambacho kina athari kubwa kwa mwananchi wa Kenya hakuna,” Omanyo alisema.
Kundi hilo la wabunge vijana maarufu kama ‘Team Ground’ linawajumuisha Babu Owino, Gathoni Wamuchomba, Ctherine Omanyo, Amos Mwago na Charles Ngusia.
Vijana wameapa kurejea mitaani tena kuanzia wiki kesho kuishinikiza serikali kuvunja bunge la kitaifa kwa kile wanadai kwamba walienda kinyume na mamlaka waliyopewa na wananchi kupitisha mswada wa fedha ambao hata hivyo ulitupiliwa mbali na rais Ruto baadae.