Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya mtandao wa kijamii wa Telegram, Pavel Durov amekamatwa.
Taarifa za vyomvo vya habari ziliripoti wikendi iliyopita kwamba Durov alikamatwa na polisi nchini Ufaransa na kuwekwa chini ya kuzuizi.
Durov alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Paris kwa madai kwamba programu yake ya ujumbe inarahisisha uhalifu ikiwa ni pamoja na utakatishaji fedha na ulanguzi wa dawa za kulevya.
Al Jazeera walieleza kwamba Hakimu anayechunguza kesi aliamuru Durov, 39, aongezewe muda kizuizini hadi Jumapili usiku, shirika la habari la AFP liliripoti, likinukuu chanzo kisichojulikana kilicho karibu na uchunguzi.
Durov anaweza kushikiliwa kwa mahojiano hadi saa 96, baada ya hapo lazima ashtakiwe au aachiliwe kutoka kizuizini.
Vyanzo vya ndani vilisema kwamba Durov alikuwa akisafiri kwa ndege yake ya kibinafsi kutoka Azerbaijan na kwamba hati ya kukamatwa kwa Ufaransa ilimlenga kama sehemu ya uchunguzi wa awali.
OFMIN ya Ufaransa, chombo chenye jukumu la kupambana na ukatili dhidi ya watoto wadogo, kinamchunguza Durov mzaliwa wa Urusi katika uchunguzi wa makosa yanayodaiwa yakiwemo ya ulaghai, ulanguzi wa dawa za kulevya, unyanyasaji mtandaoni, uhalifu wa kupangwa na kukuza ugaidi, kulingana na AFP, ambayo ilinukuu maafisa wakizungumza kwa masharti ya kutokujulikana.
Bilionea huyo wa Franco-Urusi anashutumiwa kwa kushindwa kusitisha matumizi ya programu yake kwa uhalifu.
Telegramu ilisema kwamba Durov "hana chochote cha kujificha" na husafiri mara kwa mara huko Uropa.
"Telegramu inatii sheria za EU, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Huduma za Dijitali - udhibiti wake uko ndani ya viwango vya tasnia," jukwaa lilisema katika taarifa.
"Ni upuuzi kudai kwamba jukwaa au mmiliki wake anawajibika kwa matumizi mabaya ya jukwaa hilo."
Ubalozi wa Urusi nchini Ufaransa umedai ufikiaji wa kibalozi kwa Durov na kutaka haki zake zihakikishwe, shirika la habari la serikali ya Urusi TASS liliripoti.
Ubalozi huo ulisema Ufaransa hadi sasa "imeepuka kujihusisha" juu ya hali hiyo na Durov. Wanadiplomasia wa Urusi wanawasiliana na wakili wa Durov, ubalozi ulisema.
Telegram, ambayo ina watumiaji karibu bilioni 1, iliundwa na Durov na kaka yake mnamo 2013 huko Urusi.
Durov alikimbia Urusi mnamo 2014 kutafuta nyumba mpya ya kampuni yake, akijaribu miji kama Berlin, Singapore na San Francisco, kabla ya kutua Dubai.