In Summary

• Seneta Boni Khalwale amemtaka Rais William Ruto kuiga mtindo wa masomo ya bure kama alivofanya marehemu Mwai KIbaki.

• Wabunge wamepinga fedha za kufadhili masomo kuwekwa kwenye kapu moja na badala yake masomo nchini kufanywa bure.

Seneta wa Kakamega Boni Khalwale
Image: DrBKhalwale//X

Seneta wa Kakamega Dkt. Boni Khalwale amewaomba wabunge, magavana na viongozi wengine serikalini kuhakikisha kuwa pesa zinazotolewa na wanasiasa waliochaguliwa kusaidia masomo ya wanafunzi wasiojiweza iondolewe na elimu ifanywe kuwa isiyolipiwa, akitoa mfano wa serikali ya aliyekuwa rais wa tatu wa Kenya hayati Mwai KIbaki.

Seneta Khalwale akiwa katika eneo la Malinya kaunti ya Kakamega siku ya Jumatatu alisema kuwa pesa hizo zote ziwekwe katika hazina na wizara ya elimu ili kufanikisha elimu bila malipo.

"Hii pesa yenye inamangamanga, sijui iende kwa MCA upate bursary, iende kwa MP utafute bursay, uende kwa gavana mfanye bursary haifikii watu vilivyo," alisema Khalwale.

Licha ya Khalwale kuomba viongozi wa kisiasa kukubaliana fedha hizo zote kuwekwa kwenye kapu moja, wabunge wameonyesha wasiwasi kuhusu njia ya kisheria ya kuchukua hela za kufadhili elimu kutoka kwa serikali za kauntu na kuzirejesha katika serikali ya kitaifa.

Wabunge wanadai kuwa ni heri masomo kuwa bila malipo nchini badala ya kuwepo kwa kapu la fedha za kuendesha masomo kwani hela hizo zitanyakuliwa na mabwenyenye waliosambaratisha mfumo wa sasa.

Awali, seneta wa kaunti ya Vihiga Godfrey Osotsi alisema kuwa kaunti hazina majukumu ya kufadhili masomo wa vyuo vikuu na taasisi hivyo basi zitakosa mgao kutoka serikali kuu kufadhili masomo.

Sawia, mwenyekiti wa kamati ya masomo katika bunge la seneti Joseph Nyutu katika mazunguzmo na The Star, alisema kuwa serikali za kaunti zina wajibu wa kufadhili masomo ya ECDEs na Tvets na wala hazifai kutoa basari za shule.

Aidha Khalwale alilalamikia kuwa watoto kutoka Kakamega na jamii nzima ya Abaluhya wanakosa masomo ya vyuo vikuu.


View Comments